Sign up for our newsletter!
Weekly new courses!

IJUWE SARATANI YA TEZI YA PROSTATE (PROSTATE CANCER)

Tezi ya prostate ni tezi yenye umbile la donati, iliyoko chini ya kibofu cha mkojo.Tezi hii huzungukwa na  mirija  ya mkojo na  uhusika uzalishaji wa maji maji yanayohusika na urutubishaji na usafirishaji wa mbegu za kiume (semen). Mabadiliko ya kimaumbile katika tezi dume kama; uvimbe au ongezeko la ukubwa  huleta  hitilafu katika mfumo mzima wa mkojo kutokana na ukaribu wa maumbile hayo. Uvimbe katika tezi dume husukuma  mirija ya mkojo kwa kuibana na kufanya mkojo upite kwa shida, ukwame au kuchuruzika bila kukusidia. Hali hii  humpelekea mgojwa uhitaji wa kutumia bafu mara kwa mara. Zaidi huwa vigumu kwa mgojwa  kuzuia mkojo usichuruzika  au kukwama . (Maumbile ya mwili, yamekadiriwa kulingana na nafasi iliyopo, hivyo umbile moja linapoongezeka ukubwa kinyume cha taratibu huleta hitilafu kwa mfumo mwingine jirani).

             BAADHI  YA MATATIZO YA TEZI YA  PROSTATE

  • Prostate Cancer ( Saratani ya tezi ya Prostate ) Saratani ya prostate ni saratani inayowashambulia  wanaume hasa wa umri wa miaka 50 na kuendelea.Saratani hii huweza kutibika kwa mionzi (radiation), upasuaji, chemotherapy au hormonal therapy.
  • Prostatitis (Uvimbe wa tezi ya Prostate); Hii ni hali ya uvimbe wa tezi ya prostate au eneo jirani inayosababishwa na vimelea maambukizi ( bacteria infection). Hali hii  hutibika  kwa dawa za Antibiotics  chini ya mwongozo wa daktari.

Enlarge Prostate  au Benign Prostate Hypertrophy (BPH) Ongezeko la ukubwa wa tezi ya prostate  Hali hii  hutokea kwa wanaume wengi hasa waliopita  umri wa miaka 50 na kundelea na huwa  chanzo cha kusababisha hitilafu katika mfumo mkojo. Ongezeko la size ya umbile la tezi ya prostate hufinya njia ya mkojo na hupelekea kizuizi katika mrija na kibofu cha mkojo (Chronic Bladder Obstruction) . Hali hii hutibika kwa dawa au upasuaji

         Dalili za ongezeko la ukubwa wa tezi ya prostate;

Maambukizi ya mfumo wa mkojo mara kwa mara ( Urinary Tract Infection,UTI); Mabaki ya mkojo kwenye kibofu au mkojo uliosimama kwa muda mrefu  ni chanzo cha maambukizi ya mfumo wa mkojo Mawe katika njia ya mkojo Mkojo wenye matone ya damuKukojoa mara kwa mara(mabaki ya mkojo katika kibofu hupelekea mtu kuhisi anahitaji kukojoa mara kwa mara japo mkojo unaopatikana ni kidogo sana Mkojo unaositaMkojo unaoshindikana kuzuia wa haraka na ghafla Kuvuja kwa mkojo kidogo kidogo Mkojo unaokatika katikaMkojo wa mara kwa mara usiku( Nocturia)Mkojo unaokulazimu kujikakamua

BAADHI YA VIPIMO VYA SARATANI YA TEZI YA PROSTATE

  • Prostate Specific Antigen (PSA);Kipimo hiki huchunguza  kiwango cha antigen za prostate  kwenye damu ambacho kwa mtu wa kawaida, huwa kati ya  4 mg/ml. au pungufu. Testi hii huhitaji ushauri wa daktari

.Prostate Specific Antigen (PSA);Kipimo hiki huchunguza  kiwango cha antigen za prostate  kwenye damu ambacho kwa mtu wa kawaida, huwa kati ya  4 mg/ml. au pungufu. Testi hii huhitaji ushauri wa daktari

Digital Rectal Exam ni  testi ambayo  hufanyika ili kugundua mabadiliko ya ukubwa   au hitilafu inayoleta mabadiliko katika maumbile ya  tezi ya prostateMara nyingi Prostate cancer haina dalili pale inapoanza lakini baadaye dalili zifuatazo huweza kujitokeza.

Damu kwenye mkojoOngezeko la ukubwa wa tezi ya prostateKupungua uzito wa mwiliUchovuAnemia (Upungufu wa chembe chembe nyekundu za damu)Mkojo wa mara kwa mara usikuKuvuja kwa mkojo kidogo kidogoMaumivu wakati wa kukojoa

Saratani ya Prostate yaweza sambaa katika mifupa na tishu za jirani na hata kubana mishipa ya mgongo na kuleta maumivu sehemu za mgongo,hip na pelvic .

Dalili nyingine ;

Maumivu  wakati wa kukojoa Kuhisi uhitaji wa kukojoa kwa ghaflaDamu kwenye mbegu za kiume (bloody semen)Ugumu wa kufanya tendo la ndoa au kupungukiwa na nguvu katika uwezo huoMaumivu katika utoaji wa mbegu za kiume Uvimbe katika sehemu ya miguu au hip na sehemu za uume au pelvic Kuhisi ganzi na maumivu ya mgongo, hip au miguuMaumivu ya mifupa ya mda mrefu na yasiyo na nafuu.

Anatomy and Physiology: From Science to Life / Edition 1by Gail Jenkins, Christopher Kemnitz, Gerard J. Tortora, Gerard J. Tortora, Christopher Kemnit;:http://www.cancer.gov/cancertopics/pdq/treatment/prostate/PatientNational Kidney and Urologic Diseases Information Clearinghouse web site: “What I Need to Know About Prostate Problems.”http://web.archive.org/web/20020601194638/http://www.niddk.nih.gov/health/urolog/pubs/prospro/prospro.htm#1Prostate Cancer Foundation web site: “About the Prostate.”http://www.prostatecancerfoundation.org/site/c.itIWK2OSG/b.68230/k.DAE7/What_Is_the_Prostate.htmNetter, F. Atlas of Human Anatomy, 3rd edition, Saunders, 2002.Young, B. Wheater’s Functional Histology, 4th edition, Churchill Livingstone, 2000.American Cancer Society web site: “Overview: Prostate Cancer.”http://www.cancer.org/docroot/CRI/content/CRI_2_2_1X_How_many_men_get_prostate_cancer_36.asp?sitearea(University of Texas MD.Anderson Cancer Center) 

Images

www.blackpressusa.com

ncccp.cancer.gov

www.webmd.com

See original article at Nesiwangu.

←Back to all blog posts